News
Loading...

TIZAMA TUKIO ZIMA LA SHEHE PONDA KUFIKISHWA MAHAKAMANI MOROGORO


Sheikh Ponda akiwa kizimbani wakati akisomewa mashitaka.
Sheikh Ponda wakati akifikishwa mahakamani.
...Akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro.
Baadhi ya wananchi wakiwa nje ya mahakama.
Ponda akitoka kizimbani baada ya kusomewa mashitaka.
Helkopta iliyomleta Sheikh Ponda kutoka Dar.
Ulinzi ukiimarishwa wakati Sheikh Ponda akitolewa kwenye gari ili apande helkopta kurudi Segerea.
Helkopta ikiondoka eneo hilo na Sheikh Ponda.
...Ikiwa angani.
Baadhi ya wananchi wakiangalia helkopta iliyoondoka na Ponda.
Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro na kusomewa mashitaka matatu yanayomkabili.
Ponda alifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi waliokuwa na mbwa baada ya kupokelewa kutoka katika Viwanja vya Gymkhana alipotua kwa helkopta majira ya saa tatu asubuhi akitolewa katika Gereza la Segerea, jijini Dar es Salaam.
Makosa matatu aliyosomewa Sheikh Ponda na wakili wa serikali, Bwana Bernard Kongola mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro Richard Kabate ni ya uchochezi na kutaka kuvuruga amani ambayo mtuhumiwa ameyakana.
Mawakili wa upande wa mtuhumiwa walikuwa Ignas Pungu na Bantalomeo Tarimo, wakati upande wa serikali kulikuwa na Benedict Kongola, Gloria Rwakibalila na Asnab Mhando.
Kesi hiyo itasikilizwa tena Agosti 28 mwaka huu na mtuhumiwa amerudishwa Segerea jijini Dar es Salaam kwa usafiri uleule wa helkopta.
(HABARI/PICHA: DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO)


SOURCE:GLOBAL PUBLISHERS
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment