Fadhila za Rakaa kumi na mbili za sunna
Imesimuliwa na Bibi Ummu habibah Ramla bint Abi Sufyan(Radhia Allahu anha) amesema amemsikia Mtume wa Allah(swalla Allahu alayhi wasallam)" Hakuna mja yoyote muislamu atakaeswali kwa aijli ya Allah rakaa 12 kila siku kwa kujipendekeza na si za Fardhi ila Allah atamjengea nyumba peponi” Imepokelewa na Imam Muslim.
Ndugu zangu wa kiislamu katika hadithi hii mtu anaahidiwa nyumba katika pepo ya Allah na kuahidiwa nyumba jannah ina maana ya kupata pepo ya Allah. Kaahidiwa hayo yule ambae atadumu na rakaa 12 za sunna kila siku. Rakaa ambazo sio za faradhi bali ni za kujipendekeza tu kwa Allah yaani rakaa za sunnah. Ni zipi hizo rakaa 12?Na tuangalie hadithi nyengine ya Bibi Aisha(Radhia Allahu anha) anasema " Amesema Mtume wa Allah rehma na amani ziwe juu yake " Yoyote atakaedumu na rakaa 12 usiku na mchana ataingia peponi: rakaa 4 kabla ya adhuhuri na 2 baada yake. Rakaa 2 baada ya sala ya maghrib, Rakaa 2 baada ya sala ya ishaa na rakaa 2 kabla ya sala ya alfajiri"(Imepokelewa na tirmidhy,nasai na ibn majah).
Rakaa zote hizo kila moja ina ujira mkubwa' ila kwa ujumla wao atakaedumu nazo basi mtu huyo kaahidiwa nyumba Jannah. Ni fursa ilioje baada ya mtu kumaliza kusali fardhi akatenga muda na kusali Sunna kwani katika fardhi kuna makosa mengi tunayoyafanya na ili kujaliza makosa hayo na swala angalau zikubalike mbele ya Allah basi ni muhimu kutekeleza sunna.Kuna watu wengine huwa hawana dharura yeye anapenda tu afike msikitini asali faradhi na aondoke ndugu zangu wa kiislamu panapoadhiniwa basi tukimbilieni msikitini ili tupate kufanya kheri kama hizi.Wala usione tabu kwenda kukaa msikitini kwa kuwa umekimbilia kheri.Tusiwe wepesi wa kukaa masaa mawili kusubiri mpira bila ya kufanya chochote au kukaa masaa kuangalia michezo ila kuwahi msikiti na kuswali sala za sunna tunakuwa wavivu.Tuacheni uvivu tufanye bidii za kuandaa akhera zetu. Allah atuwafikishe innahu waliyu dhaalika walqaadir alayhi.Allah ni mjuzi zaidi

0 comments :
Post a Comment