Serikali, imesema inafanya juu chini kumtia nguvuni mtu mmoja anayejiita Nabii Tito ambaye amekuwa akipita huku na kule akieneza maneno yake mwenyewe akidai ni ujumbe kutoka kwa Mungu, Amani ndiyo lina ishu nzima.
Kwa mujibu wa afisa wa ngazi za juu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye alikataa kuweka wazi jina lake, alipasha kuwa, serikali inayo habari kuwa, Nabii Tito amekuwa akisambaza vipeperushi kwenye baa mbalimbali za jijini Dar vikielezea uhalali wa mtu kunywa pombe, kufanya uzinzi na mwanaume kurithi mke wa nduguye jambo ambalo linaonekana ni la upotoshaji.
...Nabii Tito akikata kiu kwa bia aina ya Safari
Alisema kuwa, kimsingi serikali haina dini, lakini inapotokea mtu hana
kibali wala hajulikani makao makuu yake ni wapi, anapitapita kwenye
mabaa na ‘kuhubiri’ uongo hawezi kuvumiliwa.“Serikali tumekuwa tukijitahidi sana kuhakikisha kila imani inayoanzishwa nchini inakwenda kwa misingi ya maandiko ya imani hiyo na sheria za nchi pia, lakini imani nyingine zinapingana na nyingine zinazofanana nazo,” alisema afisa huyo.
...hapa akifurahia kinywaji
Aliendelea kusema kuwa, serikali inaamini Nabii Tito hana usajili wa
imani yake na kwamba, propaganda anazozieneza mitaani zinatokana na
ujanja wake wa kujitafutia ‘mkate’ wa kila siku, “ndiyo maana maneno
yake yamejaa upotoshaji mkubwa,” alisema afisa huyo.Gazeti hili lilifanikiwa kupata vipeperushi vya Nabii Tito ambaye amenukuu baadhi ya maandiko na kuyahalalisha katika mahubiri yake na kwenye vipeperushi hivyo.
Baadhi ya vipengele vya kushangaza kwenye vipeperushi hivyo ni pamoja na kile kisemacho; Mungu ni binadamu tena ni mwanaume na dhambi ya uzinzi haimhusu mwanaume.
Vipengele vingine ni vile vinavyosema kuwa, ukitumia sigara au bia ya baridi kama una hasira zinakwisha na kusisitiza matumizi ya konyagi kwa mtu mwenye kusumbuliwa na mafua.
...Nabii Tito akipigana baa
Amekwenda mbali zaidi kwenye vipeperushi vyake pale anapomwomba Mungu
abariki viwanda vyote vya pombe ili viendelee kuzalisha bidhaa hizo
ambazo imani nyingi zinapingana nazo.Kufuatia kauli za Afisa huyo wa Mambo ya Ndani, Amani lilikwenda hewani na kuongea na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Afande Suleiman Kova ambaye alisema kuwa, yeye ni mtekelezaji tu, amri ya kumtia nguvuni mtu kama huyo inatoka kwa Mkuu wa Mkoa ambaye ndiye mwenye mamlaka.
...huu ndio waraka wake
Amani likamwendea hewani Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, mheshimiwa
William Lukuvi ambaye alisema serikali inawasaka sana watu wa aina ya
Nabii Tito, wanaopita huku na kule wakijifanya manabii.Alisema lengo la usajili ni kuzijua sera za imani husika kwa kuwa wapo waliotaka kusajiliwa wakakataliwa baada ya sera zao kutoiridhisha serikali.
Alisema Mchungaji anayepita kuhubiri baa anatakiwa kuwa na kibali maalum vinginevyo atakuwa anafanya kinyume na sheria za nchi, akasisitiza:
...akisoma neno la Mungu pembeni yake akiwa na bia ya Safari
“Tena niletee ofisini sasa hivi kipeperushi cha Nabii Tito ili nianze kufanyia kazi.”Baada ya kumalizana na Mheshimiwa Lukuvi, Amani lilimpigia Nabii Tito lakini simu yake haikuwa hewani kwa siku nzima ya Jumatatu. Hivi karibuni,Nabii Tito alinaswa katika Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni akinywa ‘mma’, ilipokoa alianza kukunjana mashati na baadhi ya wateja waliokuwa wakila vyao pande hizo
0 comments :
Post a Comment