HABARI KUTOKA AHBAABUR RASUUL
Maelfu ya waandamanaji wamejitokeza mwanzoni mwa wiki hii
kupinga mashindano ya Miss World
yanayotarajia kuanza jumapili ya kesho nchini Indonesia .Waandamanaji hao wametaka
shindano hilo lifutwe kwani linadhalilisha utu wa mwanamke na ni kinyume na
mafundisho ya kiislamu.
Upinzani mkubwa toka kwa waandamanaji hao umezidi, katika
taifa hilo lenye Waislamu wengi zaidi
duniani,licha ya waandaaji kudai wameondosha vazi la ufukweni (bikini)
Baadhi ya wanaume na wanawake 800 kutoka kundi la Hizbut
Tahrir la Indonesia wamekusanyika katika mji
wa Jakarta nje ya wizara ya ustawi wa jamii, wakitoa wito kwa serikali wa kufuta
shindano hilo.
Aidha waliandamana hadi makao makuu ya shirika la habari la Indonesia
MNC kwamba liache kutangaza habari za shindano hilo lililopotoka. "Je,
tunataka nchi yetu kuonekana kama ya watu wa ngono?" mmoja wa waandamaji
alisema kwa sauti kubwa .
"Sisi tutaendelea kuandamana na kuwaambia watu jinsi ya
udhalilishaji wanawake kwa kufanyika shindano hili," alisema mratibu wa
maandamano hayo, Zikra ASRI,huku akiwa
amezungukwa na wanawake waliovaa hijabu nyeupe na baibui nyeusi.
Mjini Medani katika kisiwa cha Sumatra, wanachama 500 wa Hizbut Tahrir waliandamana
hadi majengo ya serikali, na kudai kuwa shindano hilo lifutwe.Licha ya upinzani
kuongezeka , waandaaji wamesema kuwa shindano
hilo lazima lifanyike na halita athiri heshima na utamaduni wa indonesia
Shindano la Miss Dunia linatarajiwa kuanza Jumapili katika
kisiwa cha Bali, na mshindi anatarajiwa kupatikana katika jiji la Jakarta Septemba 28.
Nchi hiyo yenye watu milioni 240,June mwaka jana mwanamuziki
Lady Gaga alilazimika kufuta onesho lake,baada ya viongozi wa dini ya kiislamu kutishia
kuchoma moto ukumbi ambao atafanyia onesho hilo,baada ya mwanamuziki huyo kuonesha
mavazi yake ya ndani.
waandamanaji nchini indonesia |
0 comments :
Post a Comment