News
Loading...

FAHAMU KWA UNDANI KUHUSU MAISHA YA KABURINI


(Yanapoanza Maisha Ya Barzakh)
↓↓↓
Maisha ya baadaye; maisha baada ya haya tuliyonayo hivi sasa hapa duniani. Na leo tutazungumzia maisha baada ya mja kufariki.
↓↓↓
Maisha hayo kuanzia mtu anapokufa huitwa ni ‘Maisha Ya Barzakh’. Barzakh ni kipindi baina ya wakati wa mauti na Qiyaamah. Na kila maiti atapitia katika maisha hayo, awe Muislam au kafiri, mwema au mwovu, na katika kipindi hicho ambako mtu anajiwa na Malaika wawili na kuhojiwa na kisha hufuatia neema au adhabu za kaburini. Inajulikana kuwa kuna makazi matatu;
↓↓↓
makazi ya Dunia (Daarud Duniya), makazi ya Barzakh (Daarul Barzakh) na makazi ya kudumu (Daarul Qaraar).
↓↓↓
Maisha ya Barzakh ni maisha yanayotofautiana kabisa na maisha ya dunia, na hakuna ajuaye hakika kamili ya maisha haya na namna yalivyo isipokuwa Allaah pekee.
↓↓↓
Maisha ya kaburini ni kile kipindi anachokaa mtu baada ya kufa kwake mpaka kufufuliwa kwake. Kipindi kati ya parapanda la kwanza ambalo ni amri ya kufa viumbe vyote na parapanda la pili ambalo ni amri ya kufufuliwa viumbe vyote vitakavyotakiwa vifufuke, Huitwa Barzakh ↓↓
Tunajulishwa kuhusu Barzakh katika Aayah ifuatayo:
↓↓↓
“Mpaka yanapomfikia mmoja wao mauti, husema: Mola wangu Nirudishe”,
“Ili nitende mema sasa badala ya yale niliyoyaacha. Wapi! Hii ni kauli aisemayo yeye tu. Na nyuma yao kipo kizuizi mpaka siku watapofufuliwa”. [Al-Mu-uminuwn: 99-100].
↓↓↓
Katika kipindi hichi cha maisha ni mambo gani yanayoendelea katika nafsi ya mwenye kufa?
↓↓↓
Wengi kwa kujiliwaza katika wakati huo hufikiria kuwa watu wanakuwa mapumzikoni. Na watu ambao hawaamini siku ya mwisho huamini kuwa kifo ndio mwisho wa maisha ya watu na iliyobaki ni kuoza na kuwa chumvi chumvi zitakazotumika ardhini.
↓↓↓↓
Katika kipindi cha Barzakh roho za watu wema zitakaa pahali pazuri kungojea malipo yao ya Peponi, Ama zile za watu waovu zitakuwa mahabusu zikingojea siku ya hukumu yao. Hivi ndio tunavyojifunza katika Hadiyth ifuatayo:
inatueleza nini juu ya maisha ya Kaburini.
↓↓↓
Bara’a bin ‘Aazib amesimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) akisema:
“Malaika wawili watamjia (maiti), Watamkalisha na kumuuliza: Ni nani Bwana wako? Atajibu: Allaah pekee Ndiye Bwana wangu. Kisha watamuuliza tena, Ni nani huyo aliyeletwa kwenu? Atajibu: Alikuwa ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam). Watamuuliza tena; Amekuleteeni habari gani? Nimesoma kitabu cha Allaah nikaamini kutokana nacho na nikaithibitisha ‘Iymaan hiyo (katika matendo)”.
↓↓↓
♣Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) akasema:
“Mtangazaji (mwenye kunadi) atatangaza (atanadi) kutoka mbinguni: Hakika mja Wangu amesema ukweli. Mtengeeni sehemu Peponi na mvisheni mavazi ya Peponi, Na mfungulieni mlango wa Peponi. Kisha utafunguliwa. Akasema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) na hewa ya Peponi na harufu yake nzuri ya ma nukato itamjia na Pepo itakurubishwa kwake kiasi cha upeo wa macho.
↓↓↓
Ama kwa kafiri
asiyeamini, ........
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) alitaja kifo chake na akasema: Roho yake itarudishwa katika kiwiliwili chake na Malaika wawili watamjia, Watamkalisha na kumuuliza: Ni nani Bwana (Mola) wako? Atajibu: Haa! Haa! Sijui! Watamuuliza tena: Ni ipi dini yako? Atajibu: Haa! Haa! Sijui! Kisha watamuuliza ni nani huyo aliyeletwa kwenu? Atajibu Haa! Haa! Sijui! Kisha mwenye kunadi atanadi kutoka mbinguni: Hakika amesema uongo, Kwa hiyo mkunjulieni kitanda cha motoni. Akasema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) Kisha joto lake na upepo wa moto utamjia na kaburi lake litakuwa jembamba sana kwake mpaka mbavu zake mbili zitapishana.
Kisha atakabidhiwa kwa Malaika kipofu na kiziwi mwenye pande (rungu) la chuma, Kama mlima ungelipigwa na chuma hicho ungelikuwa vumbi. Atampiga kwa chuma hicho kwa kipigo ambacho kitasikika kwa kila aliye mashariki na magharibi ispokuwa viumbe wa aina mbili (Majini na Watu) hawatasikia. Atakuwa vumbi na kisha roho itarudishwa tena kwake.” (Ahmad na Abu Daawuwd).

Allah atukinge na adhabu za kaburini
..............aamiin
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment