"Je, Matapishi Ya Mwanaadamu Ni Najisi?"
Tumetangulia kusema mara nyingi kwamba asili ya vitu vyote ni twahara, na kwamba havihamishwi toka kwenye asili yake ila kwa kihamisho sahihi cha kutolea hoja, kisichopingana na kile chenye kutiliwa nguvu au kuwa sawa nacho. Na ikiwa tutalipata hilo, basi ni vizuri. Na kama hatukulipata hilo, itatulazimu tusimame msimamo wa kumpinga anayedai kuwa ni najisi. Kwani kudai huku kuna maanisha kwamba Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta'ala) Amewajibisha kwa waja Wake kuviosha vitu hivyo vinavyodaiwa kuwa ni najisi, na kwamba kuwepo kwake kunazuia kuswali navyo. Basi ni ipi dalili ya hilo?!
Na matapishi na mfano wa vitu kama hivi, hakikuthibiti kwa njia sahihi
(ya kuaminika) chenye kuyahamisha toka kwenye utwahara wa asili.
Na imepokelewa kuhusu matapiko kauli ya 'Ammaar akisema: "Hakika utaosha nguo yako iliyoingiwa na mkojo, kinyesi, matapishi, damu na manii".
Lakini kauli hii ni dhaifu haitolewi hoja. Na Allah Ndiye Mjuzi zaidi.
Na imethibiti toka kwa Abu Ad-Dardaai akisema kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitapika, akafungua na akatawadha (Hadiyth sahihi: Imetolewa na Abuu Daawuud (2381), na At-Tirmidhiy (87), Ahmad (6/443) na wengineo)
Katika maelezo haya, hakuna kiashirio chochote juu ya unajisi wa matapishi, na wala hakuna dalili juu ya ulazima wa kutawadha akitapika mtu, na wala hayaonyeshi kuwa wudhuu unatenguka kwayo, bali lengo lake ni kusunisha mtu atawadhe anapotapika. Kwani kwa kitendo tu cha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), hakuonyeshi kuwa ni wajibu.
Pamoja na hayo, si kila chenye kutengua wudhuu kinahesabiwa kuwa ni najisi. Na Ibnu Hazmi amelielekea hili na akalichagua Shaykh wa Uislamu katika (Al-Fataawaa).
"Nini Hukumu Ya Majimaji (utoko) Yanayotoka Kwenye Utupu Wa Mwanamke Na Kile Kiitwacho Unyevunyevu Wa Utupu Wa Mwanamke?"
Maulamaa wana mielekeo miwili kuhusu unyevunyevu wa utupu wa mwanamke: ( Al-Mughny (2/88), na Al-Majmu'u (1/570))
WA KWANZA
Ni najisi, kwa vile mtoto haumbwi katika utupu kufananisha na madhii. Wametolea dalili kwa maelezo ya Zayd bin Khaalid kwamba alimuuliza 'Uthmaan bin ‘Affaan (Allaah Amridhie) akisema: "Nieleze, (nini hukumu) mtu anapomwingilia mkewe na wala hakumwaga manii? Akasema 'Uthmaan: "Atatawadha kama anavyotawadha kwa ajili ya Swalah, na ataiosha dhakari yake". 'Uthmaan akasema: "Nimeyasikia toka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)….". (Isnad sahihi: Imetolewa na Al-Bukhaariy (292), na Muslim (347), lakini imefutwa (mansuukh))
Na maelezo ya Ubayy bin Ka'ab kwamba yeye alisema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mtu akimwingilia mkewe na wala hakumwaga? Akasema:
(ﻳﻐﺴﻞ ﻣﺎ ﻣﺲ ﺍﻟﻤﺮﺃﺓ ﻣﻨﻪ ﺛﻢ ﻳﺘﻮﺿﺄ ﻭﻳﺼﻠﻲ)
((Ataiosha sehemu aliyomgusa nayo mwanamke, kisha atatawadha, na ataswali)) (Isnad sahihi: Imetolewa na Al-Bukhaariy (293), na Muslim (346), nayo imefutwa (mansuukh))
Wamesema: Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuamrisha kuiosha sehemu iliyogusana na utupu wa mwanamke ni dalili juu ya unajisi wa unyevu wa utupu wa mwanamke.
Mimi ninapinga (Abuu Maalik) nikisema kwamba Hadiyth hizo mbili zimefutwa (Angalia kwenye "Fathul Baary" (1/473))
na Hadiyth nyingine zenye kuamrisha kuoga kama itakavyokuja katika sehemu yake inshaAllaah.
Na pia kuna uwezekano wa kuwa amri ya kuosha ni kutokana na madhii yanayomtoka mwanamume au mwanamke.
Vile vile wametolea ushahidi juu ya unajisi wa (majimaji hayo) kwa kuwa kwake yanatoka katika moja ya njia mbili. Na kanuni inasema:
"Chenye kutoka katika njia mbili, basi ni najisi isipokuwa manii".
WA PILI
Kwamba majimaji ya utupu ni twahara (Angalia kwenye "Jaami'i Ahkaamu An-Nasaaiy" (1/68) cha Shaykh wetu Mustwafa bin Al-'Adawy Allah Amhifadhi)
Mwelekeo huu unatolewa dalili kwa yafuatayo:
1- Kwamba 'Aaishah - Allaah Amridhie,- alikuwa akiyakwangua manii kutoka katika nguo ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yakiwa yametokana na kukutana kimwili, kwani Mtume kamwe hakuota
(Hivi ndivyo alivyosema katika "Al-Mughny" (2/88). Na Shaykh wetu amesema: "Hili linahitajia matini toka katika Qur-aan au Hadiyth, na wala hatukuikuta matini katika mfano wa hili")
na ilhali yeye anakutana na umajimaji wa utupu. Na kwa vile sisi, lau kama tungelihukumia unajisi wa utupu wa mwanamke, basi tungelihukumu unajisi wa manii yake. Kwani manii hayo yanatokea kwenye utupu wake, na kwa hivyo yananajisika kwa unyevunyevu wake.
2- Kwamba majimaji haya ni jambo ambalo liko wazi, nayo huwatoka sana wanawake. Na hakuna shaka kwamba jambo hili lilikuwepo kwa wanawake katika enzi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama ilivyo kwa wanawake wa zama zetu hizi. Na wala haikupokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaamrisha kuoga (kuosha) au kutawadha kutokana na hali hiyo.
3- Kwamba kauli ya Maulamaa isemayo "Kila chenye kutoka kwenye njia mbili ni najisi isipokuwa manii", basi hii si kauli iliyopokelewa toka kwa Aliyehifadhiwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na wala kauli hii haijafanyiwa ijmaa ya Ummah.Bali imepokelewa kwamba baadhi ya vinavyotoka toka kwenye njia mbili havitengui wudhuu, kama vile damu ya istihaadha kama itakavyokuja katika mahala pake inshaAllah.
Ninasema (Abuu Maalik): Ninaloliona mimi ambalo lina nguvu, ni kwa ufafanuzi huu:
"Ikiwa majimaji haya yanamtoka mwanamke wakati wa kuchezeana na mumewe, au wakati ana hamu ya kujamiiana na mfano wa hili hasa, basi hayo ni madhii. Na mimi nimejua kwamba madhii ni najisi ambayo ni lazima ioshwe, na ni yenye kutengua wudhuu.
Ama ikiwa majimaji haya yanatoka kwenye utupu wa mwanamke takriban nyakati zote, na yanazidi wakati wa ujauzito, au wakati anapofanya kazi kwa bidii, au anapotembea mwendo mrefu, basi majimaji hayo ni twahara kiasili kwa kutokuwepo dalili juu ya unajisi wake. Na Allah Ndiye Mjuzi zaidi

0 comments :
Post a Comment